Radio Interview

Na haya unayoyaona ni kipindi cha redio kwa maandishi, ambacho kitakuwa kikirushwa kwenye stesheni mbalimbali vya redio kuanzia wiki chache zijazo. Kipindi kinarushwa na kuandaliwa na Lis Helfen, na kipindi hicho kimebeba nyimbo 5 kutoka album zangu, pia mahojiano ya moja kwa moja kati ya mimi
na Muandaaji. Karibu! Pia furahia!

Kipindi Kizima

—–~*~—–~*~—–~*~—–

(Lis)Habari za leo ndugu msikilizaji?
Karibu katika kipindi hiki maalum:
Anaeongea nawe leo hii ni mimi Elisa
kutoka Global University Tanzania:
na pia siko pekeyangu,
ila leo tunaongea na Felis Mwambalo
kuhusu maisha, tumaini na upendo.
Karibuni…

Wewe Ni Wangu

(Lis) Sawa sawa na wimbo tuliosikiliza,
Felis, Nini kilifanya uandike wimbo huu?

(Felis) Mara nyingine sisi watunzi
tunaandika nyimbo sawa na Poets
hasa wanaoandika baruwa kwa wapenzi wao.
Nami kama Poet wa Yesu au mtunzi,
niliona vyema kuandika maneno mazuri
yakumpendeza mpenzi wangu Ambaye ni Yesu.
Wakati mwengine mambo hutokea maishani,
na unahitaji mtu wa karibu kukusaidia kuyavuka.
Alie karibu yangu zaidi ya wote ni Yesu…

(Lis) Asante Felis.
Je unaweza tuambia ni wakati gani wowote
ambao Yesu alikuonekania ulipomuhitaji zaidi?

(Felis) Tangu nilipokuwa mdogo,
nilikuwa na shauku yakutumia mziki kufikisha ujumbe
Najua wote tuna shauku na maono…
Na kama wengi wenu,
sikuwa hata na namna yakufanya
maono yangu ifikie matendo au vitendo.
Ila Yesu alikuja, na kimihujiza alinifungulia njia
na nikaweza kurekodi album yangu ya kwanza, nakuizindua.
Maelfu ya watu walihudhuria,
pia wengi walitoa ushuhuda namna gani wali hudumiwa
kupitia mziki kwenye tamasha hilo.

(Lis)Asante Felis.

(Lis)Tunakukaribisha nawe ndugu msikilizaji
kuchangia maoni yako kuhusu haya tunayozungumza
kupitia internet. Kuweka mawazo au maoni yako
tembelea http://www.maoninamawazo.wordpress.com

Ebu tusikie wimbo huu
kutoka album ya kwanza ya Felis
iitwayo “ Yuko Njiani ”

Hakuna Amani

(Lis)Naamini wimbo huu unagusa maisha yetu wote.
Tunafahamu majanga yanayotokea ulimwenguni.
Wengine wetu wameshuhudia kwa karibu zaidi,
na yanazidi kuongezeka kote duniani

(Lis) Felis, Je, unaweza kutuambia baadhi ya vitu vigumu
ambavyo umewahi kukabiliana navyo maishani?

(Felis) Mambo nilioyoyapitia ni yale ya kawaida
ambayo wengi wenu pia mnapitia.
Ilifika wakati ambapo hapakuwa na chakula,
hakuna hata hela ya usafiri kufika kanisani
au kwenye huduma.
Siku nyingine niliumwa na kichwa sana
na sikuwa na uwezo wa kununua hata panadol,
na huku natakiwa kuhudumu mchana huo.

(Lis)Na jambo hilo ulilishindaje?

(Felis) Nilikuwa na imani ndani ya Yesu,
na niliamini katika ahadi zake.
Nilizidi kumkumbusha kwa habari ya aliyo yasema
katika Yohana 15:7 inayosema,
“Kama mkikaa ndani yangu, na neno langu ndani yenu;
ombeni lolote nami nitawapa.”
Basi niliomba nakuzidi kuomba, na hatimae akajibu.
Alinipa nguvu yaku tembea katika hali ngumu
na kunipeleka katika ushindi, ndipo nikaimba umenitendea.

(Lis)Tunaweza kubaliana wote
kuwa ni kweli tunapitia mambo magumu maishani,
Ila swali ni hili, unapopitia shida au tabu…
Je una mkimbilia nani kati wakati huo?

(Lis)Nadhani tutapata jibu katika wimbo huu.

Umenitendea

(Lis) Asante kwa wimbo mzuri Felis

(Lis)Je, unaweza tuambia baadhi ya mambo
ambayo Mungu amekutendea?

(Felis)Mungu amenisaidia kufanikisha shauku yangu;
kuwafikia watu wengi kupitia mziki…
Nazidi kupokea simu na ujumbe mfupi wa maandishi
kutoka sehemu mbalimbali popote nchini hata sehemu ambazo sijawahi fika,
watu wakitowa ushuhuda namna gani Mungu amekuwa
akitumia nyimbo zangu kuwagusa na kuwa hudumia.
Pia kiroho pia, amenipeleka hatua nyingine katika kumuelewa.

(Lis)Basi tusikie wimbo mwingine kabla hatuja endelea…

Tutamsifu Bwana

(Lis)I love this song!

(Lis)Felis, unaweza tuambia nini kimekupa utayari
wakutoa dhabiu za sifa kwa Mungu?

(Felis) Kweli ninazo sababu, na wala sio moja.
Kwanza, kwasababu ni agizo, kama ilivyo katika Zaburi 150:6
“Na kila mwenye pumzi na amsifu Bwana.”
Pili, kwakuwa amenitowa kwenye giza,
hadi kwenye nuru yake ya milele.
Tatu, alijitoa uhai wake kwa ajili yangu,
na sina chakumlipa kwa alicho kifanya,
nami nimejitoa dhabiu kwa ajili ya kuimba sifa zake.

(Lis)Pata ujumbe huu….

Yuko Njiani (Remix)

(Lis)Asante Felis kwa kuwa pamoja nasi leo.

(Felis) Asante sana

(Lis) Kwa heri! Tutaonana siku nyingine.

(Lis)Tunapomalizia kipindi hiki,
ningetaka ufikiri kuhusu upendo wa Yesu.
Ukisoma katika kitabu cha Yohana 3:16,
Neno la Mungu linasema
“Kwa maana jinsi hii
Mungu aliupenda ulimwengu
hata akamtoa mwanae wa pekee;
ili kila amuaminie asipotee
bali awe na uzima wa milele.”

(Lis)Msikilizaji wangu…
Je, tumaini lako ni lipi?

(Lis)Je, umewahi kuupata huo Upendo?

(Lis)Kumbuka– kwa maoni yako au wazo kuhusu tulioyaongea,
unaweza kutumia tovuti yetu http://www.maoninamawazo.wordpress.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s